Vituo vya mzunguko
Mlima wa Biblia
Katika kituo hiki, tumealika Yusufu kuja kutembelea VBS yako! Wacha mmoja wa viongozi wako avae mavazi kama Yusufu kutoka Misri, akiwasalimu wanafunzi na kushiriki nao hadithi kutoka maisha yake ya kila siku. Baada ya Yusufu kushiriki, mwalimu anashukuru Yusufu kwa ajili ya kushiriki, anasema maneno machache, na kisha kuongoza wanafunzi katika shughuli.
Mwishoni mwa muda wako, ongoza wanafunzi katika kupiga kura kwa siku. Hegemesha bango la kupiga kura kwenye ukuta. Kisha wasilisha chaguzi mbili kwa siku hiyo, na kujadili suala hilo PASIPO kuonyesha jibu sahihi au jibu kosa. Ruhusu wanafunzi kufikiri wenyewe na kupiga kura. Wanaweza kuweka saini karatasi juu ya ukuta, au kubandika kibandiko.
Darasa la Ski
Pitia kichwa cha somo na mstari wa kumbukumbu la siku. Pitisha karatasi na kuwasaidia wanafunzi wako nayo. Kila karatasi lina shughuli tano tofauti la kufurahia!
Mbele ya karatasi ina maswali mbili. Kwa wanafunzi wakubwa, kuna mchezo ya kucheza na mwenzake. Ruhusu Wanafunzi wako kuchagua mwenza na kucheza! Kisha, kuna neno la kutafuta. Kwa wanafunzi wadogo, kuna aina 10 tofauti ya vitu yaliyo jificha kwa picha ya Yusufu. Baada ya wao kupata vitu hivyo, wacha wapake picha rangi.
Kisha, pindua karatasi ili wafanye mchezo wa mlolongo. Baada ya kupata njia yao kwenye mchezo, wapake rangi ili kufanya bangili nzuri ya kuchukua nyumbani. Hatimaye, kunja karatasi na mkanda kama inavyoonekana ili kuleta mstari wa kumbukumbu nyumbani!
*Majibu ya maswali yako katika Kijitabu cha mfuko.
Kibanda cha ufundi
Katika kituo hiki, wanafunzi wako watafurahia kufanya ufundi ili kujikumbusha somo, na kuwa na kitu la kufurahia kuchukua nyumbani. Mifumo yote kwa ajili ya ufundi zinapatikana kwenye mtandao na katika kijitabu la ufundi. Kama unaweza kunakili kipande cha karatasi kwa kila mtoto, unaweza kufanya baadhi ya ufundi!
Mkahawa wa kilele
Bila shaka, unaweza kupeana vitafunio vyako vya kawaida, wakati wa chai, au chakula cha mchana, vile mumezoea. Mawazo yetu ya vitafunio, pamoja na kuwa nzuri kukula, pia ni shughuli kwa wanafunzi wako. Kila mtu katika VBS atafurahia kufanya kanzu ndefu ya Yusufu kutumia mkate au vitafunio, na inaweza kuwa inapunguza gharama pia! Zungusha viungo ili kutumia vitu unaweza kupata kwa urahisi karibu nawe, na kuwa na furaha na vitafunio.
Michezo za barafu
Kucheza ni sehemu muhimu ya maisha ya mtoto. Ikiwa ni pamoja na michezo katika VBS yako, kwa hiyo, ni muhimu! Chagua moja ya michezo miwili yaliotolewa katika kila somo, au cheza yote wawili. Husisha barafu ikiwezekana, ili kuipa VBS yako kujisikia "barafu". Uwe na furaha!
Safari za Mishenari
Kuanzisha mpango mpya, "VBS bila mipaka" ambapo kanisa lako laweza kushiriki katika kusaidia watoto katika nchi nyingine kuwa na VBS. Sisi tuna furaha kubwa kutoa hii kituo cha misioni mpya ambapo wanafunzi wanaweza pia kujifunza yote kuhusu nchi nyingine, wakati wanashiriki kuleta tofauti. Tumetengeneza vipeperushi mbili tofauti za misioni, moja kwa kila sayari. Wanafunzi wako wanaweza kufikiria wanasafiri upande mwingine wa dunia kujifunza kuhusu utamaduni, lugha, na mahitaji, na kuona jinsi VBS inavyoonekana. Watoto kutoka Marekani ya Kusini watajifunza kuhusu India, na watoto kutoka Asia ya Kusini watajifunza kuhusu Marekani ya Kusini.
Yaliyomo kwenye pakiti za misioni ni pamoja na picha za nchi au eneo fulani, karatasi la VBS katika lugha mbalimbali, na sanduku la kukusanya fedha ili kuchukua sadaka kila siku kwa ajili ya misioni.
Wasiliana na dada Kristina Krauss katika kristina@childrenareimportant.com kwa taarifa juu ya wapi utatuma mchango wako ili kushiriki katika "VBS bila mipaka." Tunashukuru michango yote sababu mahitaji duniani kote ni kubwa kuliko tunavyoweza kufanya peke yetu, na tunahitaji msaada wote tunayoweza kupokea. Unaweza pia kutumia kituo cha misioni ili kushiriki kuhusu mpango wa misioni la dhehebu lako mwenyewe na kutuma mchango wako kwa ofisi ya kwenu kwa ajili ya mradi huo.