Mapambo
Geuza kanisa lako kuwa nchi baridi ya ajabu.
Unaweza fanya hivyo!
Hata kama unaishi katika hali ya hewa ya kitropiki na kamwe huwezi kuona theluji yoyote halisi, tumia mawazo yako. Watoto hupenda kutembea ndani ya dunia tofauti!
Tafuta kwenye mtandao mawazo ya mapambo zaidi ili kufanya VBS yako ya ajabu!
Jinsi ya kutengeneza benki ya theluji
Pamoja na hatua chache tu rahisi, badilisha kanisa lako ili kwamba itakuwa kama watoto wanatembea katika dunia tofauti. Unachohitaji ni sanduku la kadibodi, karatasi au rangi nyeupe wa kufunika sanduku, na pamba au mto wa kitanda. Tengeneza moja kwa kila upande wa jukwaa.
Anza na sanduku.
Fungua upande wa sanduku na kuliweka juu ya sakafu kama ukuta ndogo.
Ambatanisha karatasi upande wa mbele wa kadibodi au paka rangi kufanya nyeupe.
Funika upande wote wa mbele wa sanduku ili iwe hakuna rangi ya kahawia inayoonekana.
Ambatanisha mto au pamba kujaza mbele ya karatasi kufanya ionekane laini. Uwache chini ya kilele bila kitu kufanya ionekane kama theluji imejaa.
Sio lazima kufunika upande wa nyuma wa ukuta wa sanduku kama itatumika juu ya jukwaa.
Maliza kufunika ukuta na pamba.
Weka kipande kubwa ya mto chini kwenye sakafu. Weka ukuta wa kadibodi kama duara kidogo juu ya pamba ulio sakafuni ili kufanya benki ya theluji.
Ili kusaidia benki kuonekana hata zaidi kama theluji halisi, basi kipande kikubwa cha pamba ininginie juu kutoka ardhi juu ya kilele cha jukwaa.
Hapa unaweza kuona benki ya theluji ikiwa na sanduku imefunikwa kwa karatasi nyeupe au rangi na mto. Waigizaji wanaweza kutembea mbele na nyuma ya benki ya theluji kusaidia kuonekana zaidi 3D. Fanya moja kwa kila upande wa jukwaa.
Mawazo zaidi za mapambo
Bonyeza kwenye picha kuona kwa karibu.
Kunja karatasi mara kadhaa, kisha kata baadhi ya maumbo kutoka pande. Funua karatasi ili kuona punje za theluji. Tengeneza maumbo kadhaa tofauti ili kuhegemesha kuzunguka kanisa. Karatasi nyembamba ni rahisi kutumia, lakini karatasi ya kawaida pia ni nzuri.
Tengeneza jina nzuri ya kadi kwa kila mwanafunzi na tawi la mti.
Shona mipira za pamba kwenye kamba na kufunga kwenye sehemu. Kisha, hegemesha kamba hizi kuzunguka kanisa.
Tengeneza duara za karatasi kisha egemeza kwenye dari.
- Pakua Mwelekeo ufundi za VBS
Tengeneza duara kutumia puto katika mlango wa kanisa kusaidia watoto kufikiria wanatembea katika nchi ya baridi.
Pamba ukumbi na karatasi bluu au nyeupe au plastiki, na kuhegemesha punje za theluji kila mahali.
Sabuni ya theluji - Hakuna uwezekano kwamba tutakuwa na theluji yoyote halisi, lakini unaweza kutengeneza vitu nyeupe za kucheza nazo. Utahitaji bidhaa kama microwave na sabuni ya mti (sabuni pekee inafanya kazi). Weka sabuni kwenye sahani kubwa ya microwave. Fungulia Joto kwa muda wa dakika mbili hadi tatu na kuruhusu wanafunzi kuangalia sabuni inavyopanuko kama wingu wa theluji. Wacha ipoe kabla ya kucheza nayo nje.
Sura ya Mlima - Tengeneza sura ya mlima na kuwasaidia watoto kuona jinsi wanajitahidi kuelekea kileleni. Andika sehemu mbalimbali juu ya sura hiyo kichwa cha ujumbe wa kila siku.
Tengeneza mlima na wanafunzi wako. Kila mwanafunzi akunje karatasi iwe koni kwa ajili ya mlima. Tumia gundi kushika pamoja na kukata chini ya koni kufanya laini. Milima mirefu yanapata barafu juu.
Weka sehemu ya picha ili wanafunzi wachukue selfies.
Tumia mawazo haya kupamba kanisa lako kwa VBS:
- Punje za theluji za karatasi
- Kamba za taa
- Puto Bluu na nyeupe
- Vitambaa za meza nyeupe
- Pambo ya Bluu na nyeupe
- Karatasi ya milima kwa ukuta
- Mitungi za Bluu na punje za theluji
Rembesha pambo zako
Fanya msimu wako wa baridi ingare zaidi, kama mfano huu wa mtu wa barafu.
Vifaa vya:
Maji
Vijiko 3 za chokaa 1 kwa kikombe cha maji
Maelekezo:
- Jaza chombo hicho na maji ya moto, ongeza chokaa, na kukoroga. Ni sawa kama baadhi ya chokaa itatua chini ya chombo.
- Kwa kutumia kamba, funga mapambo kidogo kwa penseli, kijiko, au kitu yeyote mrefu. Teremsha mapambo ndani ya maji ya moto ya mchanganyiko wa chokaa, hakikisha haiwezi gusa upande au chini ya chombo.
- Weka chombo mahali pa utulivu, na usiruhusu kitu chochote kutikisa. Baada ya masaa kadhaa, fuwele za urembo yataanza kutokea. Wacha kwa saa kadhaa au usiku wote ile fuwele zaidi yatokee. Ikiwa tayari, weka mapambo juu ya kitambaa ya karatasi ikauka kwa takribani saa moja.
- Leta kikuzi ya kioo ili wanafunzi waone fuwele!
Shusha za bure
Tafuta kwenye mtandao mawazo zaidi za mapambo ili kufanya VBS yako ya kushangaza!
Punje za theluji za rangi
Punje za gundi kwa ajili ya kushikisha madirisha za kanisa yako! Pakua faili na ununue stika za rangi yanayopatikana kwenu, au upige chapa na kukata iwe karatasi nata.
Kamba za barafu za karatasi
Tengeneza Kamba za barafu za karatasi ili kupamba jukwaa la kanisa lako! Tumia karatasi za kiwango au buni nakala ili kufanya Kamba za barafu kubwa!!
- Kupakua Mwelekeo wa VBS Ufundi kwa Kingereza