Kuhusu sisi

Watoto ni wa muhimuSisi ni akina nani

Children, conferences and training, materials“watoto ni wa muhimu” ni shirika la kanisa la kimataifa ambalo lina fikia madhehebu yote ambalo liliundwa mwaka wa 2005. lengo letu ni huduma ya watoto duniani kote likiwa na mkazo maalum kwa nyenzo.

Tuko na tofauti mbili ukilinganisha na mashirika mengine mengi.kwanza,tunaweka nyenzo zetu zote kwenye mtandao ikiwa bure kutoa kwenye mtandao.nyenzo zetu zilizo pigwa chapa zinapatikana kwa bei ya chini,lakini hatuzui kutoa nakala.tofauti ya pili haturudii nyenzo zetu mara nyingi,lakini tunaunda shule ya jumapili MPYA na mitaala ya VBS kila mwaka.

Tunapatikana saa moja toka mji wa mexico.kwa miaka kumi iliyopita,tumekuwa tukiunda nyenzo na kihispania kwa ajili ya watu wa Marekani kusini ikiwa na jina la huduma “Los Ninos Ceuntan.”katika mwaka wa 2014,tulifungua maono yetu kuhusisha dunia Zaidi na lugha ya kiingereza.katika mwaka wa 2015,tulianza kutafsiri nyenzo zetu kwa kiportuguesi,kihindi,kikanada,kimayalam na kimarathi. Tuna wafanyikazi 20,ndani na nje ,wakifanya kazi kwenye ofisi,wakiunda nyenzo,kwenye kutafsiri,kwenye duka la kupiga chapa,ama kazi kwenye uuzaji.sisi ni timu la ya wandugu na wadada ndani ya yesu,kufanya kazi kukusaidia.

Uko hapa kubadilisha maisha;tuko hapa kukusaidia

Maelezo ya mawasiliano

Otumba, Mexico State (karibu na Mexico City)
code la nchi: (52)

592-924-9041
kristina@childrenareimportant.com

Our print shopHuduma yetu

Makanisa mengi duniani yanafanya kazi kufikia kizazi kifuatacho bila raslimali za kutosha.nyenzo zetu zote kwenye mtandao ni za bure kuzitoa huko,bure kutoa nakala,na bure kutumia na kupeana. ndio.umeona vizuri ni BURE kabisa !

Kila mwaka tunaendelea kuandika na kutoa nyenzo mpya.kwa njia hio unaweza tumia kile ambacho tunacho bila kujali kuhusu kesho.kutakuwa na nyenzo mpya kabisa mwaka ujao pia,tunatoa muundo wa kufurahisha ukiwa rahisi kupiga chapa kwa muundo uutakao. si lazima utoe kwenye mtandao somo la kila wiki kwa sababu kila mtaala wa shule la jumapili umepangwa kwenye vitengo 13 vya wiki.unaweza toa kwenye tovuti na upige chapa  kitabu cha mwalimu  na kitabu cha mwanafunzi kwa kundi la umri wako na utakuwa tayari kwa miezi tatu ijayo ya madarasa.

Kwa sasa tuko na Zaidi ya wageni 1000 wa kipekee kwenye tovuti yetu kila siku,wakitoa wastani wa gigabiti 10 kila siku kutoka nchi 28 tofauti. Hii ni wastani wa vitabu 700 vinavyotolewa kwenye mtandao kila siku!na hizi nambari tunaweza kadiria kuwa mwaka jana Zaidi ya watoto million 1.5 walikuwa wanasoma kuhusu Mungu kutoka kwenye VBS na nyenzo za shule ya jumapili.Sifu Mungu!

Kwa sababu wanaohitaji ni wengi na kupiga chapa ni bei ghali sana,tuko bado na duka la kupiga chapa mexico. Tunauza vitabu vilivyo piga chapa kwa kihisipaniaKWA BEI.hatuko hapa kuunda pesa bali kushinda kizazi kijacho kwa ajili ya Yesu.kwenye mwakwa wa 2014 tulipiga chapa na kusafirisha vitabu kwa makanisa Zaidi ya 2500 kutoka madhehebu 13 tofauti,ikiwa vitabu vya wanafunzi kwa ajili ya watoto Zaidi ya 150,000.

Sehemu hio ingine ya maono yetu ni kufunza,maono,na vitendo kwa walimu ,kuwapa nafasi ya kumakinika kwa huduma ya ukweli ya watoto ambayo wanawazunguka.tunataka kukusaidia kwa miaka bila kuacha.tunajua vile ni vigumu kushinda ukifunza shule ya jumapili ama kushinda ukiendeleza ratiba ya kiamsha kinywa ama kushinda ukitafuta pesa ili uweze kununua vifaa vya huduma ya watoto wako.ni rahisi sana kutaka kuacha lakini kuna furaha ndani ya kazi na kuona matunda kwenye maisha ya watoto.tunafanya hivi kuongeza Makala,video za vitendo,na mikutano.kwa wakati huu raslimali zote za kufunzana ziko kwa kihispania,lakini tutaanza kutoa kwa wana india hivi karibuni.

Tunatarajia utapata moyo na raslimali hapa..karibu kwenye  ChildrenAreImportant.com