Watoto ni wa muhimu Kuhusu sisi Mawasiliano Shule ya jumapili Chuo cha bibilia cha likizo YanguWWC:
Mafunzo ya Kimataifa kwa Wizara ya Watoto
“Na walio na hekima watang’aa kama mwangaza wa anga; na hao waongozao wengi kutenda haki watang’aa kama nyota milele na milele.” Danieli 12:3b
MAFUNZO YA KIMATAIFA YA MTANDAONI
Moja ya shauku yetu ni maono na mafunzo kwa walimu. Hii ndiyo sababu tunaendelea kutoa vifaa vipya vya mafunzo kwa huduma ya watoto.
Kama kawaida na vifaa vyetu vyote, pakua vifaa hivi kwa bure na uchapishe nakala nyingi jinsi unavyotaka.
Mawazo mengi ya huduma ya watoto yanahitaji nyenzo fulani, lakini kitabu hiki kimejaa mawazo ambayo hayahitaji nyenzo isipokuwa mawe au majani machache.
Mungu anahitaji vipaji vyote katika mwili wa Kristo katika huduma ya watoto.Haijalishi una umri wa miaka mingapi, au una vipaji vya aina gani, au kama ulilazimishwa kufanya kazi hii kanisani... Karibu katika Huduma ya Watoto!
Katika kitabu hiki utapata muundo wa msingi wa ubunifu wa michoro, ushauri kuhusu hatua halisi kwa miradi mbalimbali tofauti, na rasilimali nyingine kwenye wavuti ili kukusaidia katika ubunifu.
Ufundi kwa vifaa vinavyoweza kutumika tena
Katika warsha hii, utapata ufundi tofauti kwa kutumia vifaa vinavyoweza kutumika tena ambavyo labda ulifikiria kutupa.
Na Kristi Krauss
Je! Unajua kwamba mikono yetu husema mengi kiasi kwamba unaweza kushiriki ujumbe bila kuzungumza?Na ndiyo sababu tutaitumia kueleza hadithi za Biblia kwa watoto wetu kwa njia mpya na inayofanya kazi.Endelea mwalimu, tunakuomba udhubutu kujaribu na kutekeleza rasilimali hizi!
Na Susana Arreola
Hebu tujifunze mawazo 15 kwa kutumia karatasi: rahisi, na inajumuisha vitendo Warsha hii itasaidia darasa lako kuwa la kufurahisha zaidi na kila wiki watoto wanaweza kurudi manyumbani kwao na ujumbe waliyojifunza kutumia shughuli hizi za kujifurahisha za karatasi. Karibu ukiwa tayari na karatasi tupu au ya kuchapishwa na uwe tayari kushangazwa!
Na Monserrat Durán
Sisi sote tunataka kuwa wabunifu zaidi katika madarasa yetu na kutumia puto kueleza hadithi ni njia nzuri ya kufanya hivyo. Katika warsha hii, tunakupa hadithi mbalimbali mbunifu za kueleza ukitumia puto mikononi mwako . Unaweza kufanya mazoezi na kuwa tayari kwa darasa lako linalofuata, hata Jumapili hii!
Hongera! Wewe ni mwalimu !!!
Sasa wewe ni sehemu ya kundi la wanaume na wanawake wa Mungu ambao wanajenga kanisa la kesho. Wewe ni sehemu ya wale wanaoweka kiburi kando na kwa unyenyekevu wanafundisha kizazi kijacho kwa sababu macho yao ya kiroho yamefunguliwa.
Na Flor Boldo
Je, ni mara ngapi kama walimu tunawaomba watoto wanyamaze kwa sababu wanapiga kelele katika darasa? Katika kitabu na warsha hii, tutafanya kinyume chake, tutajumuisha kelele na muziki kwenye somo la Biblia. Najua utadhani hili ni jambo tofauti sana! Lakini, watoto wanaweza kuendeleza uwezo wao wa kusikiliza na kupata furaha na mafundisho kwa kutumia mambo haya mawili, kelele na muziki katika darasa lako la Biblia!
Ni furaha yangu kukupa mawazo kadhaa ya jinsi ya kusherekea Siku ya Mama.
Pamoja tutapanga kuwa na wakati maalum na uliochaguliwa kwa makini ili kuwaheshimu mama zetu.
Na Flor Boldo
Unajua ni ipi sura ndefu zaidi ambayo Biblia inazungumzia na i wapi? Katika warsha hii tutajifunza mawazo inayofurahisha na ya nguvu ili kuwasaidia watoto wetu kujua Neno la Mungu; ikiwa ni pamoja na michezo, ufundi na mawazo mengine mengi ambayo utapenda. Hudhuria warsha hii na kupata darasa lako lote katika Biblia!
Kwa kawaida, lengo kuu la kufundisha shule ya Jumapili ni kuzingatia ujuzi au kuzingatia watoto, lakini kuna njia bora zaidi. Wanafunzi wa kanisa lako wanajifunza nini hasa?
Huduma ya watoto inahitaji magenerali wa nyota 5 lakini kuendeleza jeshi la Mungu inahitaji kuzingatia moyo. Tumia kifaa hiki kuhamasisha wafanyakazi na wajitolea ili kuendelea kutumikia katika huduma ya watoto, bila kuacha, mwaka baada ya mwingine.
Wahudumu wengi huzingatia watu wazima, lakini huduma yenye ufanisi zaidi ni ile ya watoto. Dada Kristina Krauss anashiriki maono ambayo mungu alimpa na inayosaidia huduma ya "Watoto ni Muhimu" ili kuzingatia watoto.
Dunia inaendelea kuwa na teknolojia zaidi na zaidi na lazima tubadilike kulingana na nyakati.` Dada Suki Kangas atatusaidia kwa vidokezo tunazoweza kutumia katika huduma za watoto wetu, kwa wale ambao wana projektar na wale ambao hawana.Huduma yako inaweza kuwa ya kisasa zaidi kwa kupitia warsha hii ya mawazo kamili.
Jifunze njia nzuri za kudhibiti darasa lako la Jumapili kupitia ratiba, nidhamu, na mawazo inayofanya kazi kutoka kwa Vickie Kangas, mwalimu wa shule na aliye na tajriba na uzoefu wa miaka mingi. Tumia hii kwa ajili yako, au toa mafunzo kwa walimu wako na kuweza kudhibiti migogoro!
Pakua seti hii nzuri ya mabango iliyo na sheria za darasa kwa vikundi vya umri mbalimbali. Imetajwa katika kitabu "Kudhibiti Migogoro" na utakuwa tayari kuendeleza huduma yako hadi ngazi nyingine!
Na Kristina Krauss
Ni wakati wa kambi! Katika warsha hii utajifunza uongozi, usalama, ufundi na mengi zaidi kuhusu safari za msitu ukiwa na darasa lako au kikundi cha watoto.Ningependa kukuhimiza kufanya jitihada za kufanya mipango ya asili na darasa lako. Wapeleke nje; na kama unaweza, lala nje kwa usiku mmoja mkiwa nao. Panga shughuli za kujifurahisha, chakula na kushirikiana nao kuhusu Mungu. Kweli hii ni njia nzuri sana ya kuunganisha mwanafunzi wako kwa Bwana wetu Yesu Kristo!
Michezo ya Fungu za Kumbukumbu
Na Kristina Krauss
Hakika unakumbuka mafungu ya Biblia uliyojifunza wakati ulipokuwa mtoto. Katika warsha hii tutajifunza michezo na mikakati ya kufurahisha ili kuwasaidia wanafunzi wako kukumbuka mafungu zaidi ya Biblia. Na tumejumuisha mafungu ya Biblia inayotupendeza zaidi kwa ajili ya kumbukumbu. Usikose!
“God has work each of us. Some He sends to the infantry and some to the army. We need teachers called to children’s ministry who will take their work seriously. We need leaders who are climbing the internal ladder so that they can, in turn, teach their students to do the same. We all need to climb a ladder – the RIGHT ladder." - Kristina Krauss, founder of Children are Important ministry.
This book is easy to read and easy to apply to your life. Don’t forget to complete the worksheet in the last chapter and write down your steps while climbing up the ranks.
Read this book for FREE in English or Pakua the English PDF (6.6 MB)
Leer este libro GRATIS en Español o Descargar el PDF en Español (1.7 MB)