Nyumba ya mabingwa

Walimu wapenzi,
Tunaomba Mungu abaraki kila mmoja wenu mkitumikia Mungu katika huduma ya watoto duniani kote. Unafanya utofauti, na kubadilisha maisha milele!

Tuna kitu cha kukushangaza. Unaweza fikiria ulikuja kuwa mwalimu wa shule ya jumapili lakini maelezo yako yamebadilika na umekuwa kocha! ndio ni ukweli, mwaka huu tutakuwa tunasoma bibilia na mandhari ya ndondi na tunatarajia kupata raha na michezo. Mwalimu mpendwa. Anza saa hii! kuwa kocha badala ya mwalimu, na itakupa msukumo kujali kwa undani kuhusu kila mwanafunzi kwenye darasa lako, na maendeleo yao wakijitahidi kuwa mabingwa.

Tutakuwa tunajifunza tunda la Roho Mtakatifu. Hata hivyo, sio kuangalia tunda la Roho Mtakatifu tu bali dhambi zetu nyingi za mwili ambazo hupigana na tunda la Roho Mtakatifu. Lengo lako nikusaidia wanafunzi wako kuwa mabingwa. Kufanya hivi, hawahitaji tu kuelewa mistari ya kukariri bali wajifunze hadithi za bibilia, lakini wanahitaji pia kuweka tunda la Roho katika vitendo katika maisha yao ya kilasiku.

Ukitumia mandhari ya ndondi, wakati wanafunzi wako katika darasa la shule ya jumapili, wacha tudhani ya kuwa wako katika mafunzo. Wanafanya kazi, na kusoma Zaidi kuhusu Mungu na jinsi ya kupigana na dhambi, kanisa lako ndio kituo cha mafunzo.

Wakati wanafunzi wako nje kwenye dunia, wako katika uwanja wa mapigano! Hapa ndipo watapigana na tamaa zao za kufanya dhambi. Nyumbani mwao, na shule, kwahivyo, ni mashindano ya ukweli na mechi za ndondi. Hii ni kwa sababu kwa kanisa, tunajua kujifanya na kupeana majibu sahihi. Tafadhali usifanye mtoto afikirie kuwa ameshinda kwa sababu ya kukariri ama kusoma katika kanisa. Hili ni funzo. Pigano lao halisi liko kwenye maisha yao. Wanaweza shinda mechi wakiweka kwenye matendo mafunzo katika wiki.

Kazi yako ya mwisho ukiwa kocha ni kuwazawadi na kuwapa motisha wanapo fanikiwa. Tayarisha tuzo kadhaa ili uweze kupeana. Wapee kumbatio ama kelele ya kutia motisha kwa kila mzunguko wa ngumi, ama mechi iliyo shindwa. Tabia unayo zawadi itakuwa tabia utakayopata kama wanafunzi wako wanakijitahidi kukufurahisha, kocha wao.

Tunatarajia unaweza kuwa na wakati mzuri ukivaa kama kocha, kurembesha darasa lako kama mahala pa kufanyia mafunzo ya michezo, na kuwa na sherehe yenye raha ya kupeana zawadi. Mafanikio ya kuishi ndani ya tunda la Roho Mtakatifu yatakuja, kama ijavyo kwenye michezo, kwa wale wako tayari kufanya kazi kwa bidii zaidi kuliko mtu yoyote. Unaweza wapa motisha wanafunzi wako kufanya kazi kwa bidii zaidi na wawe mabingwa.kuwa na Imani nao wakati hakuna mtu yeyote ana Imani nao, na utazame Mungu akifanya miujiza kwenye maisha yao.

Mungu wetu akupe motisha, unapochukua changamoto hii ya kukocha wanafunzi wako kwenye tunda la Roho Mtakatifu. Tunaomba uvunje mapungufu yote yaliyowekwa kwenye walimu wa shule ya jumapili na uwe kocha halisi katika maisha ya wanfunzi wako.

Raslimali

Shusha BURE!

Njoo uone kile tulicho nacho kwenye kurasa la rasilimali… na wakati huo huo, shusha vitabu na rasilimali zingine BURE kwa shule ya jumapili!

Soma zaidi

Logos

Chukua zana hizi za bure ili ufanye Shule ya Jumapili IONEKANE!

Weka juhudi kidogo ili ufanye darasa au eneo lako lionekane vyema na ufundi huu.

Soma zaidi

Ufundi

Watoto HUPENDA ufundi!

Ufundi hufanya darasa kuwa na furaha zaidi. Mawazo haya ni rahisi kutekeleza kutoka nchi yoyote uliko.Shusha mifano bure na kuanza kutengeneza!

Soma zaidi